HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imeanzisha huduma ya wajawazito kujifungulia katika jakuzi maalum (water birth).
Huduma hiyo inalenga inamsaidia mama kupunguza uchungu wakati wa kujifungua na kumuepusha kuchanika.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga MNH)-Mloganzila, Dk. Debora Bukuku, anasema kuanzishwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa kupanua wigo wa huduma.
Anasema kwamba awali huduma hiyo ilipatikana katika Muhimbili Upanga pekee.“Nimefurahishwa na huduma ya kujifungua kwenye jakuzi inayotolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila,” Rahel Mushi, miongoni mwa waliopata huduma hiyo.
Muuguzi Mkunga Bingwa na Mtaalam wa kusaidia kinamama kujifungua kwenye jakuzi hospitalini hapo, Rwehabura France, amesema miongoni mwa faida za mama kujifungulia kwenye jakuzi, ni ndugu atayemchagua.“Fursa ni kukaa na wataalam na kukaa naye kwa muda wote atakaokuwa kwenye jakuzi, kitu ambacho kitamuongezea faraja zaidi na kutohisi maumivu,” anasema mtaalamu huyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED