Chalamila ataja shule zilizoboronga kidato cha nne

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 08:23 PM Feb 12 2025
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Picha:Mtandao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amezitaja shule tatu za sekondari kutoka Wilaya ya Temeke ambazo zimekuwa miongoni mwa zilizofanya vibaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo.

Shule hizo ni Pendamoyo, Diplomasia, na Ndala.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, RC Chalamila aliagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha shule hizo kufanya vibaya na kuweka mikakati ya kuziboresha.

Amesema baadhi ya sababu zilizochangia matokeo duni ni utoro wa wanafunzi, changamoto za usafiri, na ukosefu wa chakula shuleni. Ameahidi kuchukua hatua za makusudi ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo.