Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita akiwa Tandahimba ameeleza kuwa kiburi, ubabe na kukithiri kwa rushwa kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na vijiji ni kwa sababu viongozi hao waliwekwa na CCM kimabavu.
“Ukiona Kobe juu ya mti siyo nguvu zake, kuna aliyempandisha. Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji wote siyo chaguo la wananchi. Siyo wawakilishi halali wa wananchi. Ni matokeo ya uporaji wa uchaguzi wa mwaka 2019 kwa hiyo hawawezi kuwahudumia wananchi, wanawasikiliza tu waliowaweka.” amesema Mchinjita.
Aliongeza kuwa ACT Wazalendo kitaendelea kupigania kuundwa na kutekeleza kazi zake kisheria kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Tunajiandaa kuipeleka Serikali Mahakamani kupinga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED