Makalla:CCM haijawahi kuiba kura na kitashinda kwa kishindo

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 07:27 PM Jun 04 2024

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makala.
Picha: Romana Mallya
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makala.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makala, amesema CCM ipo imara, haijawahi kuiba kura na kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao.

Makalla amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Boma Ng'ombe Wilaya ya Hai, mkoani hapa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

Akizungumza na wananchi Makalla amesema, "CCM  kipo imara hatujawahi kushinda kwa kuiba kura na tutashinda kwa kishindo. Mvuto wa Katibu Mkuu kuingia Kilimanjaro  tayari ngome ya CHADEMA  imebomolewa wanachama 10 wanajiunga na CCM."

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdallah Hamid anasema," Sisi hatuji kuwaambia tufanyaje tunawaambia mnasemaje, wapi bado meza yetu ina mambo mengi makubwa yaliyofanyika kuliko madogo  madogo yaliyobakia."