'Machawa' wa Ruto, wapambana kumuondoa Gachagua madarakani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:06 PM Oct 02 2024
Naibu Rais, Rigathi Gachagua.
Picha: Mtandao
Naibu Rais, Rigathi Gachagua.

WATU wa karibu wa Rais wa Kenya, William Ruto, wamewasilisha hoja bungeni jana, kumshtaki Naibu Rais, Rigathi Gachagua, wakimtuhumu kwa kuchochea chuki za kikabila na kuidhoofisha serikali.

Tofauti kati ya rais Ruto na Gachagua, zimeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Gachagua anasema ametengwa na amekanusha shutuma za washirika wa Ruto kwamba, alihusika na maandamano ya kupinga serikali mapema mwaka huu.

Pia wanadai kwamba, Gachagua amejihusisha na masuala ya ufisadi, kuihujumu serikali na kukuza siasa za kikabila.

Rais Ruto alimchagua Gachagua kama naibu wake katika uchaguzi wa 2022, wakimshinda aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga, katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Gachagua anatoka katika eneo la Mlima Kenya, Rais Ruto alijipatia wingi wa kura, ili kuibuka mshindi.

Tayari washirika wa kiongozi huyo wamefanya majaribio kadhaa ya kuzuia kura hiyo ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Wabunge wanaomuunga mkono Rais Ruto, wamesema kwamba wana zaidi ya idadi inayohitajika ya kumuondoa kiongozi huyo serikalini.

Zaidi ya wabunge 250 wanadaiwa kuunga mkono hoja hiyo ya kumtimua naibu huyo wa rais, madarakani.

BBC