Basi la timu ya Dodoma Jiji FC limepata ajali ya asubuhi hii maeneo ya Nangurukuru kuelekea Somanga mkoani Lindi likitokea mjini Ruangwa ambako jana walicheza mechi ya ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo FC.
Inaelezwa kuwa basi hilo lilipinduka mara mbili. Taarifa zinadai wachezaji wengi wamepata majeraha na hakuna kifo kilicho ripotiwa
Katibu Mkuu wa Timu hiyo, fortunatus Johnson amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba kwa sasa huduma ya uokozi inaendelea.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED