KATIBU WA NEC, Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla, amesema chama hicho kunajipanga kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa asilimia 99.999
Akizungumza leo Septemba 6,2024, na wananchi wa Karatu na Ngorongoro amesema uchaguzi huo ni msingi wa Uchaguzi Mkuu 2025.
Kwa mujibu wa Makalla,CCM iko tayari kwa uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa na uhakika wa ushindi wa kishindo kwenye sanduku la kura,hivyo ni muhimu wanachama na wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi kuanzia Septemba 11 hadi 20,mwaka huu kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa Novemba 27,mwaka huu.
"CCM imekuja kwenu kuwaeleza umuhimu wa uchaguzi huu,hakuna mradi utakaotekelezwa bila kuhusisha ardhi ya kitongoji,hivyo lazima wachague kwa mnyororo wa mfanano wa viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini ili miradi isikwame,"amesema.
"Mafanikio tuliyoyapata kwa miaka mitano yanayokana na kwamba kuanzia ngazi za vitongoji tulichagua viongozi wa CCM na kurahisisha utekelezaji wa miradi.Tunataka Ngorongoro,Karatu na Arusha iwe ya kijani,"amesema
Tunazima zote tunawasha zote maana yake CCM ing'ae katika uchaguzi huu.Najua wapo ambao mmewachoka hawatoi taarifa za mapato na matumizi,nawahakikishia CCM itawaletea wagombea safi wasio na 'makondakando' wagombea watakaowaunganisha wananchi,watawaletea maendeleo.
"Wenyeviti wa vijiji wasiosoma taarifa za mapato na matumizi,tutawaletea wanaojua kusoma taarifa hizo.Hatutaki ambao tutaanza kuwasafisha kwa madodoki na sabuni,"amesisitiza Makalla.
Kwa mujibu wa Makalla,uchaguzi huu utapeleka salamu kwa Uchaguzi Mkuu 2025,hivyo wasikiangushe chama hicho na kwamba hiyo ndio zawadi pekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametekeleza vyema Ilani ya CCM.
"Ilani yetu ndio nyenzo sahihi ya kushinda uchaguzi ulio mbele yetu.Uchaguzi wowote unashinda kwa idadi ya kura,ili tushinde tunataka asilimia 99.999 na kwamba ili kuwa na uhakika wa kura hizo ni lazima wanaCCM wawe mstari wa mbele kujiandikisha,"amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED