Aomba msaada matibabu ya Kalsiamu

By Tuntule Swebe , Nipashe
Published at 05:40 PM Feb 18 2025
Teresia Paulo
Picha: Tuntule Swebe
Teresia Paulo

TERESIA Paulo (74) mkazi wa Boko Kwampemba anawaomba Watanzania kumsaidia kupata Sh. milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu yakuongeza kalsiamu, ili kuwa na afya njema na kuendelea na majukumu yake.

Wakizungumza na Nipashe Mtoto wa mama huyo, Fatuma Athumani wanaomba wasamaria wema kuwasaidia kupata kiasi hicho cha fedha ili kuokoa maisha ya mama yao.

Amesema awali walifikiri ni ugonjwa wa kawaida  na tulimpeleka Kituo cha Afya Bunju, lakini kadiri siku zinavyosogea hali ilizidi kuwa mbaya.

Amesema walipewa rufaani ya kwenda Hospitali ya Rufaani ya Mkoa Mwananyamala ambako alifanyiwa vipimo na kutakiwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Mifupa MOI.

“Tulipompeleka MOI alipimwa na kubainika ana upungufu wa kalsiamu ndo sababu ya mifupa yake kuvunjika maeneo ya mikono na miguu,”amesema.

Amesema walielekezwa vyakula vya kula kuwa ni samaki, maziwa na uji wa ulezi, na kwamba mgonjwa alipaswa kufanyiwa upasuaji.

“Tuliondoka  hospitalini tumeshagundua tatizo lakini hatukupata suluhisho la kudumu kuwa zilihitajika fedha Sh. milioni 1.5.Tunawaomba Watanzania watusaidie kuokoa maisha ya mama yetu, chochote walichonacho ni msaada sana kwetu,”amesema Madina Sagefu mtoto wa mama huyo.

Kwa yeyote mwenye msaada wowote anaweza kuwasiliana na familia hii kupitia namba hizi 0740402725 au 0755414859