Abiria milioni 1.5 watumia treni ya mwendokasi (SGR)

By Ibrahim Joseph , Nipashe
Published at 04:51 PM Jan 24 2025
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Picha:Ibrahim Joseph
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Imebainika kuwa zaidi ya abiria 1,500,000 wamesafiri kwa kutumia treni ya mwendokasi (SGR) katika kipande cha Dar es Salaam, Morogoro, na Dodoma.

Akizungumza leo, Januari 24, katika kituo cha treni ya mwendokasi cha Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema takwimu hizi zinaonyesha mafanikio makubwa katika huduma ya usafiri wa reli ya kisasa.

Aidha, Msigwa ameeleza kuwa maandalizi ya kuanza kusafirisha mizigo kupitia kipande hicho cha reli yanaendelea vyema. "Tunakaribia kukamilisha maandalizi ya kusafirisha mizigo kati ya mikoa ya Dodoma, Morogoro, na Dar es Salaam," amesema.

Kwa mujibu wake, treni moja ya mizigo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 264 kupitia mabehewa maalum. Pia, mabehewa mengine yenye uwezo sawa tayari yamewasili bandarini kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu.