Kiongozi Mkuu wa Kundi la Hamas, Ismail Haniyeh amefariki dunia leo Julai 31, 2024 alipovaamiwa kwenye makazi yake mjini Tehran, Iran.
Haniyeh ameuawa siku moja baada ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian aliyeapishwa jana Jumanne Julai 30,2024.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (The Iranian Revolutionary Guard Corps) limesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na wanaendelea na uchunguzi.
Haniyeh (62), alikuwa mwanachama mashuhuri wa Hamas mwishoni mwa miaka ya 1980, na alichaguliwa kuwa Mkuu wa Kundi la Hamas mwaka 2017.
Taarifa za kifo cha Haniyeh, zimeripotiwa ikiwa ni muda mfupi tangu Israel itangaze kumuua kamanda wa Hezbollah wakidai ndiye aliyehusika na shambulio katika milima ya Golan na kuisababisha Israel kurudi nyuma kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED