Vodacom yamtunuku Wakala Bora wa Kanda ya Kati

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:08 AM Feb 08 2025

Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania, Epimack Mbeteni, amemkabidhi zawadi na cheti Thabit Juma Idd kwa kutambua mchango wake kama wakala bora aliyefanya vizuri zaidi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa kampuni ya Vodacom kwa Kanda ya Kati.
Pigapicha Wetu

Katika jitihada za kusogeza huduma karibu na wateja na kuwaelimisha zaidi kuhusu huduma zao, viongozi wa Vodacom kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam walifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya kanda hiyo. Ziara hiyo ililenga kuzungumza na wateja, kutatua changamoto zao papo hapo, pamoja na kutambua mawakala waliotoa huduma bora zaidi.

Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika Wilaya ya Manyoni, jijini Dodoma, na kuhudhuriwa pia na Meneja Mauzo wa Vodacom Wilaya ya Manyoni, Bernard Kombe, pamoja na Afisa Mauzo wa M-Pesa wa Kanda hiyo, Musa Kushoka.