Samsung kuimarisha ubunifu wa AI na matumizi ya kidijitali Tanzania

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:17 PM Jan 23 2025
Mgope Kiwanga, Meneja biashara wa simu za mikononi Samsung Tanzania.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mgope Kiwanga, Meneja biashara wa simu za mikononi Samsung Tanzania.

Katika kuashiria ujio mpya wa teknolojia ya simu zinazotumia akili mnemba (AI), Samsung imekuja na toleo mpya la simu zake za kisasa za Galaxy S25 katika soko la Tanzania.

Wakati Tanzania ikiharakisha ajenda yake ya mabadiliko ya kidijitali, toleo hili mpya la simu linakuja na uwezo wa hali ya juu wa AI, vipengele vya kisasa, na suluhisho za kibinafsi zinazolenga kuwawezesha watumiaji, kuimarisha uunganisho, na kusaidia kuendeleza maono ya taifa ya ukuaji wa kiteknolojia. 

Kwa kuunganisha ubunifu wa AI katika maisha ya kila siku, vifaa hivi ni hatua muhimu katika kuziba pengo la kidijitali na kukuza jamii iliyounganishwa zaidi na yenye tija.  

Zikiwa na Mfumo wa Snapdragon 8 Elite, simu hizi zinatoa nguvu ya kipekee ya ufanyaji kazi wa kifaa. Teknolojia hii inawezesha injini ya ‘ProVisual’ ya kizazi kipya, ambayo inatoa utendaji wa juu wa kamera na udhibiti, na kuifanya kuwa simu pendwa kwa wapenda picha na watumiaji wa teknolojia.  

Manish Jangra, Kiongozi wa Timu ya Samsung Tanzania, alionesha kufurahishwa na uzinduzi huo, “Matoleo ya simu hii ni mseto wa teknolojia ya hali ya juu ya AI na vifaa vya kisasa. Imeundwa kubadilisha jinsi tunavyopata uzoefu wa teknolojia katika maisha yetu ya kila siku. Vifaa hivi vinatoa uzoefu wa AI ulio salama na wa kibinafsi unaolingana na mahitaji na mapendeleo ya mtumiaji. Kuleta teknolojia hii bunifu katika soko la Tanzania ni hatua kubwa, inayowawezesha watumiaji kufurahia uwezo usio na kikomo wa Galaxy AI.”  

1

Vifaa vipya vya kampuni hiyo ya simu vinawaletea watumiaji msaidizi wa AI anayebadilika kulingana na mapendeleo yao huku ukiwahakikishia faragha. Kwa uwezo wa hali ya juu wa kuelewa lugha ya kawaida, vifaa hivi vinawawezesha watumiaji kutumia simu zao kwa njia ya moja kwa moja, kama vile kutafuta picha maalum au kurekebisha ukubwa wa fonti kwa urahisi. Aidha, AI inayotambua muktadha wa matumizi inarahisisha kazi nyingi kwa wakati mmoja na inatoa mapendekezo yanayofaa kulingana na mahitaji ya mtumiaji.  

Ndani ya simu hizi, Snapdragon 8 Elite inatoa ongezeko la asilimia 40 katika utendaji wa NPU, asilimia 37 kwa CPU, na asilimia 30 kwa GPU ikilinganishwa na toleo lake lililotangulia. Uboreshaji huu unahakikisha utendaji mzuri hata kwa kazi ngumu za AI, ikiwemo uhariri. 

“Kwa simu hii mpya ya kisasa, tunawawezesha Watanzania kufanikisha mambo mengi zaidi katika maisha yao ya kila siku. Ni mchanganyiko kamili wa teknolojia ya AI ya hali ya juu na vifaa vya kiwango cha kimataifa vinavyoendana na kasi ya maisha ya kila siku,” anasema Mgope Kiwanga, Mkuu wa Biashara wa Samsung Tanzania.  

Ahadi ya Samsung kwa uendelevu inaonekana wazi katika mfululizo wa Galaxy S25. Kila kifaa kina betri zilizotengenezwa kwa angalau asilimia 50 ya kobalti iliyorejelewa, inayopatikana kutokana na vifaa vya zamani vya Galaxy na michakato ya uzalishaji. Juhudi hii inaonesha kujitolea kwa kampuni hiyo kupunguza athari kwa mazingira na kukuza matumizi ya rasilimali zinazozunguka.

2