Nchi 8 kushiriki maonesho ya nishati, umeme jadidifu

By Gwamaka Alipipi , Nipashe
Published at 12:14 PM Feb 07 2025
Mkurugenzi Mtendaji ya Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) Oscar Kissanga (Wa tatu kutoka kushoto) akiksta utepe katika ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya nishati jadidifu wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa TAREA, Matthew Matimbwi.
Picha: Gwamaka Alipipi
Mkurugenzi Mtendaji ya Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) Oscar Kissanga (Wa tatu kutoka kushoto) akiksta utepe katika ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya nishati jadidifu wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa TAREA, Matthew Matimbwi.

NCHI nane kutoka Afrika na Ulaya zinatarajia kushiriki maonesho ya kwanza ya teknolojia ya nguvu ya nishati na umeme jadidifu, lengo likiwa ni kuinua na kuongeza bunifu kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), Matthew Matimbwi alisema maonesho hayo ni ya kwanza nchini Tanzania, yameletwa kwa ushirikiano wa TAREA na kampuni ya ETSIPL kutoka nchini India.

Alizitaja nchi zinazoshorolo ni kutoka Afrika, Afrika Kati na Ulaya ikiwemo nchi ya Tanzania, Zambia, Ulaya wa Falme za Kiarabu (UAE), Kenya, India, China, Afrika Kusini, Ujerumani.

Alisema kuwa maonesho hayo yana lengo la kukuza biashara ya teknolojia kwa wafanyabiashara wa kitanzania katika sekta ya nishati safi endelevu na kukuza masoko ya ndani na nje ya nchi ikiwemo kujitangaza kimataifa na kuweka biashara kwenye viwango vya juu.

“Wafanyabiashara wa Tanzania watapata fursa kubwa sana kupitia maonesho haya kwani hapa kuna kampuni zaidi ya 100 kutoka nchi hizo nane ambao watabadilishana uzoefu na kukuza uwezo zaidi,” alisema.

Alisema maonesho hayo yamelenga bidhaa kama vile nyaya, betri, taa, nishati mbunifu, elektroniki, usambazaji, uwekaji vifaa vya majumbani, UPS, mifumo ya majumbani, HVAC, ikiwemo na mawasiliano ya simu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA), Oscar Kissanga alisema maonesho hayo yataweza kuwasaidia Watanzania kukuza masoko hasa kuelekea soko la Afrika ikiwemo bidhaa za kilimo, madini pamoja na kuwafundisha kujitangaza zaidi.

Mmoja wa washiriki katika maonesho hayo, Nafsa Shabani kutoka kitabu maalumu cha kuweka anuani za kampuni (NCD) alifafanua kitabu hicho kinasaidia kampuni Za kibiashara, viwanda kuweka kumbukumbuku na anuani zao, kuwezesha wapatikane kiurahisi hasa pale katika kujitangaza kutafuta masoko ndani na nje ya nchi.

Alisema kitabu hicho kinatoka kwa mwaka mara moja kipindi cha Machi kwa kulipia gharama nafuu elekezi kwa anayehitaji, kwamba kitabu hicho kinasambazwa kwenye hoteli zote ndani na nje ya nchi, balozi na viwanja vya ndege ili waweze kufikiwa kwa urahisi.