Shina Tarime Group CCM lazinduliwa, wamchangia Samia fomu ya urais

By Romana Mallya , Nipashe Jumapili
Published at 02:04 PM Jun 02 2024
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali, Tarime Group lenye wanachama 200, lililoko eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Picha: Romana Mallya
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali, Tarime Group lenye wanachama 200, lililoko eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amezindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali, Tarime Group lenye wanachama 200, lililoko eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, ambalo limemchangia Rais Samia Suluhu Hassan Sh. 50,000 ili kuchukua fomu ya urais.

Dk. Nchimbi amewasili Arusha, tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwenye mikoa mitano, ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia  Abdallah Hamid.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Hussein Khamis, amemweleza Katibu Mkuu huyo kuwa wameamua kumchangia Sh. 50,000 Rais Samia Suluhu Hassan ili kuchukua fomu ya urais 2025.

Naye, Balozi Nchimbi amesema CCM kitawachangia Sh. milioni mbili kama walivyoomba na kumteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuwa mlezi wa shina hilo ambaye naye amemuhakikishia Katibu Mkuu kuwa utekelezaji unaanza mara moja.