Kuelekea Yas Kili Marathon 2025 Wanariadha, makocha mguu sawa

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 04:19 PM Feb 18 2025
Kocha wa mchezo huo, Andrew Panga.

WAKATI ikiwa imebaki wiki moja kabla ya kufanyika mbio za Kilometa 21 za Yas Kili Marathon 2025, baadhi ya wanariadha na kocha wa mchezo huo wameelezea maandalizi yao kuelekea mbio hizo.

Kocha wa mchezo huo, Andrew Panga amesema vijana wapo tayari kwa ajili ya mbio hizo.

Mmoja wa wanariadha watakaoshiriki mbio hizo, Elibariki Zephania, amewapongeza wadhamini wa kilometa 21, Kampuni ya Yas kuwa kuboresha mbio hizo.