TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), watatoa huduma upimaji bure kwa wakazi wa Mbeya.
Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote kwa watoto na watu wazima tarehe 17 - 21/02/2025 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika viwanja vya City Park Garden mkabala na uwanja wa mpira wa miguu Sokoine jijini Mbeya.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano JKCI, Anna Nkinda, amesema hay oleo, kwenye taarifa kwenda kwa umma na kwamba kutakuwa na wataalamu wa lishe, watakaotoa elimu itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha.
“Elimu itakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza (NCD), na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
“Hii ni tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la ‘Dk. Samia Suluhu Hassan Outreach Services’. Uytafanyika upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa washiriki wa mkutano wa 109 wa Wadau wa Elimu kwa Umma na wananchi wa mkoa wa Mbeya,” amefafanua.
Amesema watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu na yatakayohitaji matibabu ya kibingwa watapewa rufani ya kuja kutibiwa katika JKCI, Upanga jijini Dar es Salaam.
“Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo, ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED