Wazazi, walezi msiwaachie walimu pekee malezi

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 12:30 PM Aug 29 2024
Wazazi, walezi msiwaachie walimu pekee malezi
Picha: Mpigapicha Wetu
Wazazi, walezi msiwaachie walimu pekee malezi

OFISA Elimu Msingi Kata ya Mikocheni, Elizabeth Lulagora amesema wazazi na walezi, wasiuache mzigo wa ulezi kwa walimu pekee, kwa madai kwamba wapo ‘bize’ kutafuta fedha za mahitaji ya familia.

Lulagora, akimwakilisha Ofisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, aliyasema hayo hivi karibuni kwenye mahafali ya 18 kwa wahitimu watarajiwa wa darasa la saba katika shule ya St. Florence, Dar es Salaam.

“Mtoto usimtengeze kwa elimu tu, mara nyingi watoto wana tabia za wale wanaoshinda nao na kuwahudumia nyumbani, kama vile hausigeli au jamaa zetu.

Watoto nao wana msongo wa mawazo wanahitaji wasikilizwe. Mnakaa nao? Katika kata yangu kuna mtoto alikuwa anachelewa shuleni na Mwalimu Mkuu wake akaamua kwenda kumtembelea. 

Kufika nyumbani kumbe mtoto alikuwa anaenda kuvuta bangi kwanza alafu anasubiri apate hewa harufu itoke, ndio aende shule. Mwingine wa miaka 16 alimwambia mamake nataka kuacha shule niolewe kapata mchumba!

Mama akamfanyia ushauri, akaelewa. Kuolewa ikaahirishwa. Pia kuna mambo ya ukatili wa kijinsia kwa miaka minne nikiwa ofisi ya Kata hii, nimebaini ukatili wa kwanza unaanzia ngazi ya familia,” alisema Lulagora.

Pia akisisitiza wazazi na walezi kuzungza na watoto wao wanataka kuwa na taaluma gani maishani, Ofisa elimu Wilaya Kinondoni na si kusubiria kuingia katika taaluma kwa dharura. 

1

“Ni vizuri kuanza kuwaandaa watoto wajue na wakae katika kile wanachokipenda. Mzazi anarudi kalewa anaimba watoto hawalali, mzazi mkali na maneno ya kukasirisha mengi, inamtengenezea mtoto kupata magonjwa ya akili,” alisema.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Wilson Kakamga alisema mahafali hayo ni ya 18 yakiwa na wanafunzi 82 kati yao wavulana ni 45 na wasiachana 37.

“Haikuwa kazi rahisi kwani wengi walianza tangu wakiwa ‘baby class’ (darasa la watoto). Shule ilianza mwaka 1993 ikiwa na wanafunzi wanne. Sasa tuna watumishi 107. Shule ina ufaulu unaongezeka,” alisema Mwalimu Mkuu huyo.
2

Alisema wazazi na walezi wakumbuke ulinzi wa mtoto ni jukumu la kila mmoja na wazazi wachukue jukumu hilo kwa kujiunga na walimu kupinga ukatili.

“Wazazi kukaa mbali na watoto kwa kutowafuatilia mwenendo wao baadhi inapotokea mtoto anatabia mbaya majibu ya mzazi ni kwamba mtoto amepata tabia hiyo shuleni, jambo ambalo si kweli tushirikiane katika malezi.

Kundi la mwaka huu wahitimu ni miongoni mwa waliobora katika nidhamu. Shule ina wanafunzi zaidi ya 900. Muundo mpya wa mitihani katika mtaala mpya ni mzuri na wanafunzi wamemudu mabadiliko,” alisema.

“Kuelekea tarehe 11 na 12 Septemba mtihani wa taifa wa darasa la saba. Changamoto ni upatikanaji wa kufundishia lugha ya kiingereza ni changamoto tunaomba serikali isaidie, viwe vinapatikana mapema,” alisema Mwalimu Mkuu.
3