Bunge la Kenya lamwondoa madarakani Naibu Rais

By Allan Isack , Nipashe
Published at 10:27 PM Oct 08 2024
 Rais wa Kenya,Rigathi Gachagua,
Picha: Mtandao
Rais wa Kenya,Rigathi Gachagua,

HATIMAYE Bunge la Kenya,limemuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya,Rigathi Gachagua, kutokana na mashtaka 11 yaliyokuwa yanamkabili ikiwamo la ufisadi na kuendeleza ukabila akiwa ni kiongozi wa Serikali.

Mashtaka mengine ni pamoja ukiukaji wa Katiba ya Kenya,kutokumheshimu Rais na kwenda kinyume na Sera za Serikali.

Bunge hilo la Kitaifa la Kenya limeidhinisha Gachagua kuondolewa madarakani baada ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Katika kura zilizopigwa kuamua hatma yake, wabunge 281 waliunga mkono hoja ya kumuondoa kiongozi huyo madarakani, huku wabunge 44 wakipiga kura ya kupinga na mbunge mmoja akikataa kupiga kura.

Awali kabla ya kura hizo, kupigwa Naibu Rais hiyo, aliweka matumaini yake kwa Wabunge waliojiandaa kupiga kura kuhusu hoja yake ya kuondolewa madarakani.

Gachagua alisema anaheshimu na anaamini Bunge litafanya uamuzi sahihi.

Naibu huyo, alikuwa akiwahutubia wabunge alipofika mbele ya Bunge kujibu tuhuma zilizowasilishwa kwenye hoja yake ya kuondolewa madarakani.

"Angalia, tafakari, na tumia dhamira yako na ufanye uamuzi yanayofaa," alisema.

"Ninaheshimu sana Bunge na uwezo wake wa kufanya uamuzi sahihi." Kiongozi huyo alitetea hatua yake ya kuzungumzia madai hayo siku moja kabla ya kufika mbele ya Bunge.