“Serikali inatekeleza Ilani kwa vitendo,” Waziri Lukuvi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:39 PM Sep 19 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Williamu Lukuvi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Williamu Lukuvi amesema ujenzi na uimarishaji wa wa miundo mbinu ya Maji Kata ya Mbezi ni kielelezo tosha kinachoonesha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo.

Waziri ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ambapo ametembelea na kujionea Mradi wa Maji Mshikamano ulipo Kata ya Mbezi Katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar e salaam na baadae kufanya Mkutano wa hadhara Mburahati, jana.

Shida ya maji Kata ya Mbezi ilikuwa tatizo kubwa hivyo kukamilika kwa Mradi wa Maji niliotembelea   kwa 100% utahudumia watu zaidi ya laki mbili.

“Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ametegua kitendawili hicho kwa Wananchi wa Ubungo kupata Maji safi na salama ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hivyo niwape shime Wananchi muendelee kutangaza kazi njema zinazofanywa na Serikali,” alisema Waziri Lukuvi.

Kazi hizi zinazofanywa na Serikali zinapaswa kuonekana na kutangazwa ili Watanzania wengine waone kazi mbalimbali kwa mifano na Falsafa ya Mhe. Rais ya Kazi iendelee  inaendelea kutekelezwa kwenye miradi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji  Prof. Kitila Mkumbo Ubungo amesema kupitia mradi wa Metroplitan Development Project (DMDP) Awamu ya Pili utajenga kingo za Mto Gide na Mto China huko Makurumula.

Aidha kwa kupitia Mradi wa (DMDP) kwa upande wa Ubungo kuna barabara 21 zitakazojengwa ikiwemo barabara nne kubwa katika Kata ya Kimara ambazo ni barabara ya lami Suka, Barabara ya Mlingo, barabara ya Milenia ya tatu, alisema Waziri Kitila.

Naye  Issa Mtemvu Kibamba amesema Wilaya ya Ubungo ilikuwa na wastani mdogo wa upatikanaji wa maji, lakini Mhe. Rais amechukua kilio cha wakazi wa Ubungo na leo miradi imekamilika.

“Serikali haikuwaacha Wananchi wa Goba na viunga vya Salasala katika ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita zaidi ya milllioni sita eneoTegeta A hivyo tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt Samia,” alisema Mtemvu

Wabunge tumepata bahati tunaomba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo Serikalini na tunazipata, ahadi yetu ni kuendelea kumunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

3

Awali Mkuu wa wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa na zuri kwa kuleta miradi ya maendeleo ambayo imechagiza mabadiliko makubwa kwa sekta mbalimbali.

Wananchi wa wilaya ya Ubungo wana deni kwa Rais kutokana na kazi kubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyofanya na Serikali ya Awamu ya Sita, kwa dhamira ya kweli na ya dhati.
“Hakuna Kata ambayo haijaguswa kabisa kwa upande wa mradi iwe ni upande wa Elimu, Maji, Barabara Afya au Miradi mengine ya Maendeleo” alisema, Mkuu wa wilaya Bomboko.