Prof. Mkenda azindua nyumba pacha za walimu

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 12:19 PM Oct 05 2024
Prof. Mkenda azindua nyumba pacha za walimu
Picha: Mpigapicha Wetu
Prof. Mkenda azindua nyumba pacha za walimu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua nyumba pacha ya walimu wa Shule ya Sekondari Lubonde, iliyopo kata ya Lubonde, wilayani, Ludewa Mkoa wa Njombe.

Amesema hatua hiyo ni kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia kwa kujenga nyumba za waliokuja, shule, madarasa na kununua vifaa vya katika shule za  sekondari na za mafunzo ya amali.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, amesema kuwa Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan, ameazimia kuboresha mazingira ya walimu nchini.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamoga, amesema kata hiyo haikuwa na shule ya Sekondari hadi mwaka 2022 ndipo serikali ilipotoa fedha, kwa ajili wa ujenzi wa shule hiyo.

Mbunge huyo ameongeza kuwa wananchi wa kata hiyo kwa hamu kubwa ya kuwa na sekondari walitoa eneo bure pamoja na kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo na nyumba ya walimu, jambo ambalo lilisaidia kuwa na bakaa ya fedha.

Mkuu wa Shule hiyo, Willy Chaula, amesema serikali kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Sekondari (SEQUIP), ilitoa Sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba  hiyo.

Chaula amesema ujenzi wa nyumba hiyo umepumguza changamoto ya walimu kukaa mbali ya eneo la shule na kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi, kwa kuwa walimu wapo karibu na eneo la shule.