Msafara wa St Anne Marie Academy wawa kivutio Ubungo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:08 PM Nov 01 2024
Msafara wa mabasi ya shule ya St Anne Marie Academy ukizunguka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam kufurahia matokeo ya darasa la 7 ambapo wanafunzi 140 wa shule hiyo wamepata alama A.

SHULE ya St. Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, imeendelea kufanya maajabu kwenye mitihani ya darasa la saba ambapo mwaka huu wanafunzi wake 140 waliohitimu darasa la saba wamefaulu kwa alama A.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura wakati wa msafara wa shule hiyo wenye magari 40 ya shule hiyo yaliyobandikwa matokeo ya shule hiyo mwaka huu yalizunguka maeneo mbalimbali za Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakiongozwa na gari la polisi na kuwa kivutio kwa watu wengi.

Ndyetabura amesema kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), wanafunzi 140 wa shule hiyo wamepata wastani wa alama A na wanafunzi 15 tu ndiyo wamepata alama B.

“Tunasherekea matokeo ya darasa saba tulikuwa na wanafunzi karibu 150 na karibu wote wamefaulu kwa alama A tunawapongeza wanafunzi ambao wametuamini na kutupa watoto wao na tunaomba waendelee kutupa watoto wao kwasababu matokeo wameyaona,” alisema

Wananafinzi wakifurahia matokeo hayo na Mkuu wa shule hiyo Gladius Ndyetabura kabla ya kuanza kwa msafara huo leo Ijumaa.

Aidha, Ndyetabura ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya elimu aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa namna walivyokuwa wanapambana kuwafundisha wanafunzi hao usiku na mchana na hatimaye kupata matokeo mazuri ambayo ni ya kujivunia.

Alimpongeza Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza kwa namna ambavyo amekuwa akiwawekea mazuri ya kufundishia iikiwemo maabara ya kisasa na maktaba yenye viyoyozi.

“Wanafunzi wa St Anne Marie Academy wanakula milo mitano kwa siku ni shule wachache sana zinazoweza kumudu kulisha wanafunzi wake mara tano kwa siku, tuna shamba laa mboga mboga kwaajili ya wanafunzi, tuna maji ya na umeme wa uhakika kwa hiyo tumekamilika tunamshukuru sana Dk Rweikiza,” amesema
Msafara wa mabasi ya shule ya St Anne Marie Academy ukizunguka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam kufurahia matokeo ya darasa la 7 ambapo wanafunzi 140 wa shule hiyo wamepata alama A.

Kuhusu siri ya mafanikio hayo, Ndyetabura amesema ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Dk. Rweikiza katika miundombinu kama madarasa, mabweni, mabasi ya shule, maktaba iliyosheheni vitabu na walimu wenye weledi ambao wamekuwa wakifundisha kwa ari kubwa.

“Wakati NECTA ilipokuwa na utaratibu wa kutaja shule zilizokuwa zikifanya vizuri kitaifa  tulikuwa tunashika namba nne, nafasi ya sita, nafasi ya nane na kuna wakati tulikuwa wa kwanza kitaifa na kwa matokeo haya tuliyopata  mwaka huu kama wangetangaza huenda ungekuta tuko 10 bora kitaifa,” amesema
Wananafinzi wakifurahia matokeo hayo na Mkuu wa shule hiyo Gladius Ndyetabura kabla ya kuanza kwa msafara huo leo Ijumaa.