HALMASHAURI ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo imetenga sh. Milion 800 kwa ajili ya uwekezaji wa taa za barabarani.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ramadhani Possi alipokuwa akizungumza kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana Novemba 13 mjini humo.
Possi alisema maeneo yatakayowekwa taa hizo ni pamoja na Ruvu darajani, Mdaula, Kibindu, Ubena na Miono.
Katika hatua nyingine Possi alisema vyumba viwili vya Madarasa vilivyolengwa kufanyiwa ukarabati shule ya Msingi Mindu tulieni havitafanyiwa hivyo badala yake vitajengwa upya.
Mkurugenzi huyo alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Diwani wa Lugoba Rehema Mwene alipohoji kuhusiana na sh. Miln tatu zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati wa vyumba viwili vya Madarasa shule ya Msingi Mindutulieni
Possi alisema sh. milioni tatu zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati sasa zitatumika kuanza kujenga msingi wa vyumba hivyo na baadae utaratibu wa fedha za kumalizika utafanyika.
Awali akifungua kikao Cha Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo aliwataka watendaji kuhakikisha wanasimamia makusanyo ya mapato yaweze kufikia lengo lililowekwa.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED