Kongamano la wanawake Kibaha lafana, wajipanga uchaguzi mdogo na mkubwa

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 08:04 PM Sep 23 2024
Kongamano la wanawake Kibaha lafana, wajipanga uchaguzi mdogo na mkubwa
Picha:Mpigapicha Wetu
Kongamano la wanawake Kibaha lafana, wajipanga uchaguzi mdogo na mkubwa

MAMIA ya Wanawake wa Kata ya Tumbi Halmashauri ya Mji wa Kibaha wameshiriki katika kongamano la Wanawake lililofanyika Mwanalugali likiwa na lengo la kuhimiza ushiriki wa Wanawake katika chaguzi zijazo ikiwemo Serikali za Mitaa.

Mlezi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha mjini Selina Koka amesema kongamano hilo ni kwa ajili ya kuwahamasisha Wanawake kugombea nafasi za uongozi na pia kujiunga na vikundi Ili waweze kunufaika na mikopo.

Selina ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini amesema kila mwezi Septemba kata hiyo itakuwa ikifanya kongamano kuwakutabisha Wanawake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo.

Pia amesema mbali ya kata ya Tumbi kata nyingine pia zitafnya makongamano kama hayo ambayo yanasaidia Wanawake kukutana pamoja na kujadilia mipango yao ya kuwakwamua kiuchumi kupitia vikundi walivyonavyo.

Akizungumza na Wanawake walioshiriki kongamano hilo kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Kibaha Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zayb Vullu amesema wanatakiwa kuhamasishana kugombea nafasi za uongozi.

Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza  viongozi Wanawake kwenye mitaa yetu na Vijiji katika uchaguzi unatarajia kufanyika Novemba mwaka huu.

1
Vullu pia amewakumbusha wananchi kuchagua  viongozi bora sio bora kiongozi ambao watawasaidia kuvuka kwenye mapambano ya kiuchumi.

"Tukachague viongozi bora kwasababu ndio tunaweka misingi ya mitano tena kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan hayo ndio malipo yetu kwa Rais amefanya mambo mengi ambayo ni neema kwa wananchi, amemtua mama ndio kichwani na mengine mengi kwenye Jamii," amesema.

Pia amepongeza Mlezi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kibaha mjini kwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii huku akimuomba kusaidia kuandaa andiko la mradi litakaloenda kwenye Taasisi za fedha ambalo litakalokuwa msaada na Wilaya nyingine katika kuwakwamua Wanawake kiuchumi.