Dereva wa TPA na wenzake 7 washtakiwa wizi wa mafuta Lita mil 9.9

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 06:19 PM Oct 22 2024
Watuhumiwa wa makosa ya Wizi wa mafuta ya Petroli na Dizel yaliyokuwa yakishushwa katika Meli, wakitoka Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusomewa mashtka 18 ya wizi pamoja na Makosa ya utakatishaji fedha wa zaidi ya Bilioni 20.
PICHA:IMANI NATHANIEL
Watuhumiwa wa makosa ya Wizi wa mafuta ya Petroli na Dizel yaliyokuwa yakishushwa katika Meli, wakitoka Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusomewa mashtka 18 ya wizi pamoja na Makosa ya utakatishaji fedha wa zaidi ya Bilioni 20.

DEREVA wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ,Tino Ndekela na wenzake saba, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka 20 liliwemo la wizi wa mafuta ya Petrol na dizel zaidi ya lota milioni 9.9 na kuisababishia hasara Kampuni ya Kimataifa ya kuhifadhi Mafuta (TIPER) Tanzania ya zaidi ya sh bilioni 26.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni  mfanyabiashara Fikiri Kidevu, Amani  Yamba, Mselem Abdallah , Kika Sanguti, Twaha Salum, Gaudence Shayo na Hamisi Hamisi, ambao walisomewa mashitaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki.

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao  na wakili wa serikali Cathbert Mbilingi ambapo alidai walitenda makosa hayo kati ya Januari mosi mwaka 2019 hadi Desemba 31 mwaka 2022, eneo la Tungi, Kigamboni , Dar es Salaam.

Akiwasomea mashitaka hayo ilidaiwa kwamba, wanakabiliwa na mshitaka mawili ya uharibifu wa mali wanayodaiwa kutenda kati ya Januari mosi mwaka 2019 na Desemba 31 mwaka 2022 Kigamboni ambapo waliharibu bomba la kusafirishia mafuta aina ya petroli na Dizel mali ya kampuni ya Tiper.