CBT yainua vyama 100 vya ushirika, wakulima 5,000 wawezeshwa kulima kisasa

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 06:56 PM Oct 22 2024
CBT yainua vyama 100 vya ushirika, wakulima 5,000 wawezeshwa kulima kisasa
Picha: Mpigapicha Wetu
CBT yainua vyama 100 vya ushirika, wakulima 5,000 wawezeshwa kulima kisasa

WAKULIMA zaidi ya 5,000 kutoka katika vyama vya ushirika zaidi ya 100 wametajwa kujiinua kiiuchumi na kuachana na kilimo cha mazoea kwa kufuata kilimo cha kisasa chini ya uwezeshwaji na ulimishaji kutoka Benki ya Ushirika Tanzania (CBT).

Wakulima hao ni wa mazao ya Kahawa na Karosho kutoka katika mikoa ya Mtwala na Kilimanjaro huku mikoa mingine yenye mazao ya kimkakati ikiwemo Tumbaku, kahawa, korosho na mazao mchanganyiko.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi hundi ya Sh.milioni 10 kwa Umoja Vyama vya Akiba na Mikopo (SCCULT), katika maadhimisho ya siku ya ushirika duniani yanayoendelea mkoani Mwanza, Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya CBT, Prof.Gervas Machimu alisema lengo ni kuhakikisha wainua vyama vya ushirika pamoja na wakulima.

Alisema pamoja na mambo mengine wamedhami maadhimisho hayo yanayoendele kwa siku nne yakitarajiwa kufungwa Oktoba 24, 2024 na Spika wa Bunge Dk.Tulia Akson.

1

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Ushirika kutoka CBT, Yahya Kiyabo alisema lengo uwkezaji katika ushirika ni kuhakikisha wanabadili kilimo kutoka katika kilimo cha mazoea na kulima kisasa.

Alisema katika kipindi cha kuanzia 2020 hadi 2024 zaidi ya Sh.bilioni 10 zimewekezwa katika kilimo  kuporesha upatikanaji wa pembejeo, ujenzi wa maghara pamoja na mashamba ya kisasa.

“Wakulima zaidi ya 5,000 kutoka katika vyama vya ushirika zaidi ya 100 vimewezeshwa kupitia mikopo pamoja na maboresho mbalimbali tangu zikiwa benki za ushirika za Tandahimba na Kilimanjaro ambazo zimeungana na kuipata CBT ambayo ilianza utendaji wake Oktoba 1, 2024,” alisema Kiyabo.