Mzize akipotezea kiatu, awaza ubingwa wa nne

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 09:04 AM Feb 07 2025
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize (jezi ya kijani), akipambana kuwania mpira dhidi ya mchezaji wa KenGold, Komanje Sandale, katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam juzi
Picha: Mtandao
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize (jezi ya kijani), akipambana kuwania mpira dhidi ya mchezaji wa KenGold, Komanje Sandale, katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam juzi

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize, amesema mabao anayoyafunga ni kwa ajili ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo na kamwe hafikirii tuzo ya mfungaji bora.

Juzi, Mzize alifunga mabao mawili katika  ushindi wa magoli 6-1 dhidi ya Kengold FC kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kufikisha mabao tisa.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mzize anayewindwa na timu mbalimbali a nje ya Tanzania, alisema kama wachezaji wanajituma uwanjani kuhakikisha wanaisaidia timu yao kutetea ubingwa.

"Kikubwa ni ubingwa kwa timu, ligi ni ngumu na kila mchezaji anapambana kuhakikisha malengo ya klabu yanatimia, tumeingia mzunguko wa pili, mzunguko wa lala salama, kila mechi ni fainali kwetu kwa sababu tunataka kuona mwisho wa msimu timu inatetea ubingwa," alisema Mzize.

Aidha, mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa (Twiga Stars), alisema suala la tuzo binafsi kwake ni jambo la pili baada ya ubingwa kutua kwa Yanga.

"Nafunga kuisaidia timu kutwaa ubingwa, suala la mfungaji bora nadhani litatokea lenyewe, mimi binafsi lengo ni kusaidia timu kutetea ubingwa tunaoushikilia," Mzize aliongeza.

Tangu mwaka jana nyota huyo amekuwa akihusishwa na baadhi ya klabu za Afrika Magharibi wakihitaji huduma yake jambo ambalo Yanga bado haijatoa baraka ya kuondoka kwa sasa licha ya ofa nono zilizowasilishwa.

Mzize, anatajwa kutakiwa na CR Belouizdad na MC Alger zote za Algeria pamoja na Mzize akipotezea kiatu, awaza ubingwa wa nne inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi.