Simulizi ya mjamzito apasuliwa kwa mwanga simu, wafa mama na mwana

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:37 AM May 09 2024
news
Picha: Mtandaoni
Mkuu wa hospitali iliyokumbwa na balaa, Dk. Chandrakala Kadam, akihudumia wagonjwa wake.

KATIKA hospitali ya manispaa huko Bhandup, East Upnar, Mumbai, mjamzito alifanyiwa upasuaji wa kujifungua (CS) kwa kutumia mwanga wa tochi ya simu baada ya umeme kukatika. Yeye na mtoto walipoteza maisha kwenye yao kutokana na upasuaji huo.

Familia ya Ansari, ilijiandaa kusherehekea mwaka mmoja wa ndoa na kuzaliwa kwa mtoto, lakini ghafla ikakumbwa na huzuni, ambako matukio ya uzembe wa wauguzi na madaktari  umetawala.

Khusruddin Ansari, baba wa mtoto mchanga aliyekufa, akatazama kamera nakusema: “Mtoto anapozaliwa hushuka chini hadi tumboni chini, lakini mtoto wa mkwe wangu alikuwa kifuani na madaktari wawili walikuwa wakijaribu kumsukuma chini kutoka juu.

“Mtoto wetu alikufa tumboni wakati huo. Walimpeleka kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya upasuaji na kisha wakatoka ili kupata saini ya mwanangu kwenye hati kwani mambo yalienda vibaya.

"Wakati mkwe wangu alipochukuliwa, umeme ulikatika. Lakini waliendelea kumfanyia upasuaji wa kujifungua wakitumia mwangaza wa tochi ya simu . Binti yangu na mjukuu wangu walikuwa tayari wamekufa."

Sahidun na Khusruddin Ansari walikuwa anatarajia kufanya sherehe ya maadhimisho ya kwanza ya harusi yao tarehe 15 Mei

Khusruddin ana mguu mmoja. Familia nzima ya Ansari ilikuwa na furaha kwani ndoa yao ilipangwa baada ya muda mrefu na habari njema ya kupata mtoto ingekuja ndani ya mwaka mmoja.

Katika kipindi cha miezi tisa, wanafamilia wanaeleza kwamba, muda wote anafanyiwa uchunguzi, alikuwa na afya njema.

 MZIZI WA TATIZO

Sahidun Ansari, mwanamke mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa Mumbai, alilazwa hospitalino hapo, saa 8. 00 asubuhi Aprili 29 kwa ajili ya kujifungua, daktari akamchunguza mzazi na kusema angejifungua kwa njia ya kawaida.

Hata baada ya saa 12 jioni, harakati hazikusimama, hivyo ndugu walimuuliza daktari tena. Daktari anasema itachukua muda, kwani ni mtoto wa kwanza.

Baada ya muda kusonga, daktari alisema mama na mtoto wako katika hali nzuri na wanazidiwa na maumivu, jamaa na wanapowaomba madaktari kufanya upasuaji wa kujifungua. 

Hata hivyo, familia inasema kuwa daktari akasema kuwa uzazi wa asili utafanyika kwa saa moja hadi saa moja na nusu.

Lakini jamaa hao wakaisema kwamba ikiwa ana maumivu, mfanyie upasuaji wa kujifungua. Walidai kuwa daktari hakusema chochote kuhusu hilo.

Wakasimulia, mgonjwa walimpatia chai na biskuti kwa ushauri wa daktari na jioni, kiwango cha moyo wa mtoto kilikuwa 110. Daktari akaahidi wanaweza kuhitimisha uzazi huo kwa njia ya upasuaji.

Rehmunnisa, shangazi wa Sahidun, aliarifu kuwa daktari huyo alimpasua kwa wembe Sahidun, bila ruhusa ya jamaa zake na kumpasua kwa lazima. Damu nyingi ilitoka mwilini mwake.

Anarejea maelezo mengine ya daktari, kwamba kiwango cha moyo wa mtoto kilikuwa pointi 40, hali inayolazimisha kufanyika upasuaji.

Mwili wa mzazi ulivuja damu sana, anasimulia Rehmunnisa akaongeza na baada ya hapo, wakamwambia wampeleke kwenye chumba cha upasuaji. 

Anasimulia, hapakuwapo shangazi zake au wauguzi kutoka hospitali hiyo wakati wa kumpeleka huko na nguo yake ilijaa damu. 

"Nilipoona haya yote nilikuwa na hofu na nilitokwa na machozi. Daktari aliniomba niondoe nguo yake. Alinipa mkasi wa kurarua nguo yake iliyokuwa imejaa damu.

“Hawakuwa na kiti cha magurudumu au kitanda cha kumpeleka kwenye chumba cha upasuaji. Tukishikilia nguo nyuma yake, tulimbeba hadi kwenye chumba cha upasuaji. Wakati huo huo, umeme wa hospitali ulikatika," anaeleza Rehmunnisa. 

Anaendelea: "Sahidun alikuwa na maumivu makali...baada ya upasuaji huo, wakati mtoto wa kiume alipotolewa, baba yake aliitwa na kuambiwa kuwa afya ya kijana huyo ilikuwa mbaya...mtoto alikuwa amekufa, lakini walimficha.

"Baada ya muda walifika na kusema kuwa mtoto huyo amefariki. Baada ya hapo mama huyo alipelekwa hospitali nyingine.’

Inaelezwa, hawakuwa na watu wa kumhamisha mgonjwa kwenye gari la wagonjwa. Ni watu wa familia ndio walifanya kazi hiyo, kwenye gari la wagonjwa hawakuwa na hata hewa ya oksijeni..

"Tulipowauliza, walisema alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kwa kweli, alikufa hospitalini. Hata hivyo, binti yetu alipelekwa katika hospitali ya Sion. Alitangazwa kuwa amekufa huko."

WENYE MAMLAKA

Ofisa Mkuu wa Afya wa Manispaa Mumbai, Daksha Shah, anasema wameunda kamati ya madaktari 10 wataalamu kutoka hospitali tatu kubwa, wakipewa wiki moja kuwasilisha ripoti, kwa ajili ya hatua kuchukuliwa. 

Inaelezwa hospitalini hapo penye mkasa, siku hiyo umeme ulikatika kila mara katika eneo lote na kuhusu mbadala wa kutumika mwanga wa tochi ya simu katika upasuaji, kukifafanuliwa;

"Timu yetu ilishughulikia hali hiyo vizuri. Siku hiyo hiyo, wafanyakazi wetu walitengeneza mwingine wa asili. Tunajaribu kutoa vifaa mbadala wa umeme kwa ajili ya kutoa mwangaza."

Agruti Patil, aliyekuwa mkuu wa idara hiyo penye mkasa, anakiri kumekuwapo na matukio ya uzembe wa madaktari katika hospitali ya Sushma Swaraj Prasrutigriha.

Patil anasema; "Hospitali ya Manispaa haina vifaa. Licha ya malalamiko ya mara kwa mara, hakuna hatua zinazochukuliwa. Nilifika huko saa 12.30 jioni siku ambayo tukio hilo lilitokea na nilikuwa hospitalini hadi saa 4.50 asubuhi. 

‘Baada ya simu za mara kwa mara, mkuu wa hospitali saa nane na nusu asubuhi, alifika huko. Jenereta katika hospitali haijatumika tangu tarehe 27 Aprili. Pia tumelalamika kuhusu suala hilo kwa serikali."

Jagruti Patil anasema, umeme ulikatika mara saba tangu asubuhi ya siku ya tukio hilo.

Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Chandrakala Kadamm, anakubali makosa hayo ya kiutendaji na ameshawaandikia barua wafanyakazi wake wahusika.

Mhandisi Umeme, Mayur Bhagwat, kutoka idara husika serikalini anakana kuhusika kwamba: wizara yao haihusiki na umeme wa hospitali.’

Anaendelea: “Hatujui nini hasa kilichosababisha kukatika kwa umeme katika eneo hilo na ikiwa jenereta ya hospitali imewashwa au imezimwa."

 

·     Kwa mujibu wa BBC