HADI sasa moja kati ya miradi miwili muhimu na mikubwa kitaifa inatekelezwa, ikiwamo ya umeme- Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Sehemu ya mitambo ilianzishwa na mingine ni inatarajiwa kuanza kazi karibuni, kama ilivyoahidiwa na serikali.
Ni mradi ambao ulipoanzishwa, ulikutana na hoja kinzani kuhusu hatima ya usalama wa mazingira, lakini serikali ngazi ya juu ikautolea ufafanuzi kuhusu usalama na faida zinazotarajiwa.
Baada ya kuingia uongozi wa serikali awamu ya sita, ndiyo ikachukua hatua ya uendelezaji kwa hatua zaidi hadi kufikia hatua sasa kwenye uzinduzi.
Kama ilivyo kawaida duniani kote, mfumo wa uendeshaji serikali kidunia, huendana na mamlaka za utekelezaji kisekta na maeneo maalum, ikiongozwa na safu ya mawaziri, ambako katika mfumo wa nchini wanasimamiwa na mtendaji mkuu serikalini, Waziri Mkuu.
Ni kwa mara nyingine, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akaziagiza wizara tano ziazohusiana kwa karibu kisekta na Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, huku akisisitiza uhifadhi wa mazingira katika vyanzo vya maji vinayojaza Mto Rufiji, inayohusiana na Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Katika orodha hiyo, Rais akazielekeza wizara za; Kilimo, Uvuvi, Maji Mazingira na Ufugaji, alipoziambia ziketi kuketi na kutumia nafasi zao Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, kupata ufanisi wake, pia umuhimu wa mto huo kimaendeleo.
Ni agizo lake rais, katika tukio la kufungua ujazaji maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere, akisema sekta zote zenye nafasi ya kuvuta wawekezaji na kutengeneza fursa kutokana na maji ya Bwawa la Mwalimu Nyerere, zifanya hivyo, zikiwamo sekta Kilimo na Maji ambazo ni wanufaika wa moja kwa moja.
"Nazielekeza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Ardhi na TAMISEMI na mamlaka nyingine mkapime maeneo hayo na muyaweke katika mashamba makubwa kwa ajili ya kufanya mnada wa wazi kwa wawekezaji wa uhakika katika kilimo.
“Nawasihi, pia mtenge maeneo maalum kwa ajili ya wakulima wadogowadogo hasa wa maeneo hayo yatakayokuwa na miundombinu ya umwagiliaji maji" akasema Rais Samia
Aidha, Rais akawa na maagizo yanayoilenga Wizara ya Mazingira, ambako anakufahamu vyema na alishawahi kuisimamia zamani kwa ngazi tofauti, kabla ya kuwa rais, akitaka zichukue hatua dhidi ya waharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji, mito na maeneo muhimu yanayotumika kama chanzo cha maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere
"Manufaa ya bwawa hili katika nyanja zote yanawezekana tu, kama tutatunza mazingira katika vyanzo vya mabonde ya mito inayoleta maji mabwawani. Hapa nataka nisisitize umuhimu wa ‘tunza mazingira’, kwani huu mradi tumeujenga kwa gharama kubwa na kwa kujinyima vitu vingi muhimu.
“Itakuwa ni dhambi kubwa kama hautatimiza malengo yake kwa sababu ya uzembe na ubinafsi wetu kwahiyo kulinda mazingira na kulinda mradi huu sasa ni suala la kufa na kupona," akatamka Rais Dk. Samia
Ni katika nafasi hiyo, aliyekuwa Waziri wa Nishati wakati huo, January Makamba, pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la umeme, TANESCO Maharage Chande, akasema serikali inaendelea na mipango ya muda ya mrefu ya kukabiliana na changamoto ya umeme.
Hapo katika orodha hiyo inajumuisha kujengwa mabwawa manne pamoja na kuanzisha miradi mingine kupitia nishati jadilifu, ili kukabiliana na changamoto ya umeme.
"Tupo katika kupanga mbele na ukiangalia ile chati yetu sisi leo hii tunajua mpaka 2040 mradi gani utaingia kwenye gridi, tumejipanga kwa muda mrefu na sio kwa muda mfupi, tunachoomba ni subira tatizo la kukatika umeme litaisha...” alisema.
Hadi sasa, ni wastani wa mwaka mmoja na nusu tangu agizo lake Rais Dk. Samia, picha ya kazi za mjumuiko unapaswa kuanikwa kwa umma kilichofanyika, kuhusiana na fahari yao umma; Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Eneo mojawapo mahsusi katika utekelezaji agizo hilo la Rais, linasimama katika mazingira na manufaa ya kiuchumi, kazi inayopaswa kufanyika kutoka kwa wataalamu wa kiwizara na serikali kwa upana wake, hata inapobidi inavuka mchango wa nje ya serikali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED