Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mnara wa Mashujaa uliopo mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya siku ya Mashujaa itakayofanyika Julai 25 mwaka huu.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mnara huo leo, Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi na amemtaka mkandarasi ambaye ni Suma JKT kukamilisha ujenzi kwa viwango na ubora ifikapo Julai 22 mwaka huu.
Naye, mshauri elekezi kiongozi, Dk. Ladislaus Mrema, amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa eneo hilo la mnara unajumuisha ujenzi wa uwanja wa gwaride, ngazi, njia za watu wenye mahitaji maalum na kitako cha mnara na bustani eneo la kuzunguka mnara.
Amesema ujenzi huo unaendelea vizuri mpaka sasa mradi umefikia asilimia 84.
Siku ya Mashujaa itafanyika Julai 25, mwaka huu mkoani Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED