Watoto wabainika korodani zao zinapanda

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 08:11 PM Jun 27 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi.
Picha: Beatrice Shayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi.

Watoto 10 wa Mkoa wa Arusha wamebainika korodani zao zinapanda badala ya kushuka chini jambo ambalo hawataweza kuwa na watoto watakapokuwa wakubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, aliyasema hayo leo wakati akiwahudumia wananchi waliojitokeza kupatiwa matibabu jijini Arusha.

Amesema kwa familia za watoto hao hawana uwezo watakusanywa na kusafirishwa pamoja kwa ajili ya matibabu ya upasuaji.

Janabi alisema kuna baadhi ya fedha za Rais Samia zilizobaki zitatumika kuwatibia watoto hao 10 na kurejea katika afya njema.