KAMANDA Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amewataka vijana kuachana na tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta mafanikio kutokana na waganga hao kuwatuma viongo vya binadamu ili afanikiwe kimaisha.
Ngonyani ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari inayohusu mafanikio ya jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi Aprili, ambapo amesema hali hiyo husababisha taharuki katika jamii kutokana na vijana hao kufanya mauaji ili wapate viungo vya binadamu.
Sambamba na hilo jeshi la polisi limekamata watuhumiwa 115 wanaojihusisha na makosa mbalimbali ikiwemo waganga wakienyeji wanaopiga ramli chonganishi.
Aidha polisi mkoani wa Katavi inaendelea na upelelezi wa tukio la watu watatu wa familia moja kudaiwa kuuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, tukio lililotokea katika Halmashauri ya Tanganyika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED