RAIS Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causal) na Chuo Kikuu cha Anga Korea (KAU) kwa kutambua mchango wake katika mabadiliko ya sera na uongozi wa kimantiki.
Shahada hiyo imetolewa leo katika hafla maalum iliyoandaliwa na chuo hicho na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Korea na Tanzania.
Hii ni shahada ya heshima ya tano wa Rais Samia baada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha Jawaharial Nehru cha India na Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, wote wakitambua mchango wake kwenye nyanja mbalimbali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED