Fred Lowassa: Balozi Nchimbi ulimtendea haki Lowassa 2015

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 12:51 PM Jun 02 2024
Mbunge wa Monduli, Fred Lowassa.
Picha: Romana Mallya
Mbunge wa Monduli, Fred Lowassa.

MBUNGE wa Monduli, Fred Lowassa, amemshukuru Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kuwa alimtendea haki baba yake, Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) na kwamba hataona aibu kusema na kama atakuwa amekosea basi asamehewe.

Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Makuyuni, wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Amemweleza kuwa, "Siku ile ulitoka katika kikao cha Kamati Kuu kwa heshima ukasema 'kwa kuwa kanuni za chama zimekanyangwa sitavumilia'.

Wewe ni Katibu Mkuu ukasimamie zisikanyagwe tena,"alimwomba.

2015 Nchimbi alitoka katika Kamati Kuu Dodoma akiwa na wajumbe wenzake na kupinga kuvunjwa kwa kanuni wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais CCM.