KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi, leo Jumapili Mei 12, 2024, ameshiriki misa takatifu na sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Katoliki jijini Dodoma, Padri Wilbroad Kibozi.
Misa hiyo imefanyikia katika Kituo cha Hija cha Kanisa Katoliki, Miyunji, Mbwanga, jijini humo na kuhudhuriwa na maaskofu, mapdari, watawa na viongozi mbalimbali wa dini, kiserikari na kisiasa akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango.
Askofu Kibozi aliteuliwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francisko Februari 12, 2024 baada ya kukubali ombi la Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Beatus Kinyaiya la kutaka msaidizi wa shughuli za kitume katika Jimbo hilo.
Askofu Kibozi ambaye hadi uteuzi unafanyika alikuwa ni Makamu Gambera na Profesa wa Seminari kuu ya Familia Takatifu, Kahama, alizaliwa Aprili 30, 1973 kata ya Lumuma, Wilayani Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma.
Askofu Kibozi aliwahi kuwa Paroko Msaidizi wa Lumuma (2010 -2012), Mkurugenzi wa Miito Jimbo Kuu la Dodoma (2012-2014) na Muunganishi katika nyumba ya malezi Livorno, Italia (2017-2019).
Pia amehudumu kama Mkufunzi wa Waseminari katika Chuo Kikuu cha Jordan, Morogoro (2019-2020) kabla ya kuwa Makamu Gombera@ katika seminari kuu ya Mwendakulima, Kahama.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED