ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Michael Lekule Laizer amesema hakuna diwani wa wilaya hiyo alishinda kwa kusaidiwa na serikali bali ni kwa kuchaguliwa na wananchi kwenye sanduku la kura.
Kiongozi huyo ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Longido,amesema eneo hilo ni ngome ya CCM na hakukua na lazima ya kutafuta kubebwa,na kwamba kiongozi huyo aliwavuruga na kuwa na migogoro mingi.
"Sisi ndio tumewachagua,kama wamepita bila kupingwa ni sisi tumewachagua,wilaya ya Ngorongoro,Longido na Monduli ni ngome ya CCM na kwamba madiwani wanashinda kwa halali na kwa asilimia 100,tunauhakika hata uchaguzi ujao tutashinda kwa kishindo,"amesema.
"Mimi ni mwanzilishi wa wilaya hii (Longido) ,vijiji vyote, kata zote nazifahamu vizuri sana,"amesema Laizer ambaye pia ni Mjumbe wa siasa Wilaya ya Longido.
Amesema maneno yaliyotolewa na aliyekuwa DC Marco Ng'umbi, ni yake na kwamba hayana ukweli bali yalilenga kuwqdhalilisha madiwani hao.
Kwa mujibu wa Laizer, amesema aliyetangulia hakuwa na uhusiano mzuri,hivyo kazi kubwa aliyonayo ni kirejesha uhusiano mwema mwenye wilaya hiyo.
Akizungumza na wananchi hao katika eneo la Kilimahewa Kata ya Mundarara, Mkuu mpya wa Wilaya, Salum Kali, amesema amejipanga kuwatumikia wananchi na kwamba namba yake ya simu anayogawa kwa wananchi itapatikana saa 24,na kwamba muda wote wamwambie kero na atawafikia.
"Naomba niwahakikishie wilaya yenu ipo salama.Kero zenu nimezisikia suala la daraja Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) watakuja,pia mmesema kuna shida ya zahanati na kituo,"amesema.
Nitapita kijiji kwa kijiji,serikali inapaswa iwepo itatue kero zenu,mmesema mnashida ya malisho mimi ni mwakilishi wa Rais Samia Suluhu Hassan, nitahakikisha nasimamia vizuri na kutatua kila kero,ni wajibu wetu kama viongozi wa serikali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED