Balozi Nchimbi aanza ziara ya kishindo mikoa mitano

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 10:59 AM May 29 2024
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.
Picha: Maktaba
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, leo ameanza ziara katika mikoa mitano akianzia Singida kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya  Idara ya Uenezi, Mafunzo na Itikadi, imesema kwamba, katika ziara hiyo,  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makala pamoja na Katibu wa NEC,  Siasa na Uhusiano wa kimataifa  (SUKI),  Rabia Hamid, nao watakuwapo.

Ziara hiyo itahusisha pia, mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambayo ni Manyara, Arusha na Kilimanjaro na kuhitimisha Mkoa wa Tanga, Juni 9, mwaka huu.