Askofu Dk. Malasusa awapa agizo viongozi wa dini, kuisaidia mahakama

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 03:16 PM May 22 2024


Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT).
Picha: Mpigapicha Wetu
Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT).

ASKOFU Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema viongozi wa dini wana kila sababu ya kuwashauri watu kwa sababu uwezo wanao na watu wanawaamini na pia wanafursa kuzungumza nao na kuwapatanisha bila kwenda mahakamani.

Askofu Malasusa amesema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia, Temeke akiwa ameambatana na wakuu wa majimbo yote sita ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani na wachungaji kwa lengo la kujifunza na kubadilishana mawazo kuhusiana na utendaji haki.

Amesema kituo hicho kina Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama Kuu jambo ambalo limeweza kusaidia wananchi kwa karibu, Mahakama ya Tanzania imefanya kitu kikubwa katika mnyonyoro wa kutoa haki na pia wamefurahishwa na 
kuwepo na kitengo cha Mahakama ya watoto, kumbe na watoto nao wanapewa nafasi ya kupata haki zao.

Askofu huyo amesema ushauri huo utawasaidia sana waumini katika masuala ya familia hasa ya ndoa na mirathi, migogoro mingi imetokea kwa sababu ya hayo masuala.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia kilichopo Temeke, Dar es Salaam, Jaji Mwanabaraka Mnyukwa akizungumza na wakuu wa majimbo sita ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wachungaji na watumishi wa kituo hicho (hawapo pichani), kuhusiana na changamoto wanazozipata katika mashauri ya mirathi na ndoa katika kusuluhisha.

"Tumejifunza kwamba hapa upo msaada wa kisheria kwa watu ambao wanakosa nguvu ya kifedha ya kuweka mawakili lakini pia tumekuta ustawi wa jamii ambao wao pamoja na mambo mengine wanatoa ushauri na wakati mwingine wanashauri watu kuondoa kesi mahakamani nankuwapatanisha,"amesema Askofu Malasusa 

Kwa upande wake, Jaji Mnyukwa amesema kituo hicho kinahusika moja kwa moja na utatuzi wa masuala ya familia na katika utatuzi huo mahakama pekee  wasingeweza ndiyo maana wanashirikiana na wadau mbalimbali na nyinyi mkiwa mkiwa miongoni mwao.

Pia, amesema kinahusika na mirathi na ndoa kwa njia moja au nyingine viongozi wa dini mnakutana na wananchi katika majukwaa mbalimbali ambayo yanasaidia katika utatuzi wa migogoro.

"Kituo chetu kwa takwimu kwa kipindi cha Januari hadi Aprili mwaka huu kituo kiliweza kutoa jumla ya hati za talaka 444 ukiangalia wingi wa idadi ya ndoa ambazo zinavunjwa katika kituo hiki, tunawaomba muendelee kuzungumza na waumini wenu kabla hawajafika mahakamani ili kupunguza mgogoro huu,"alisema Jaji Mnyukwa 

Naye, Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho, Alfred Mvungi amewaomba viongozi hao wa dini kuongeza muda wa mafunzo ya ndoa kanisani iwe hata miezi kadhaa kwa sababu migogoro mingi wanayokutana nayo inaonekana bado mafunzo ya muda mrefu yanahitajika.


Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia kilichopo Temeke, Dar es Salaam, Jaji Mwanabaraka Mnyukwa akizungumza na wakuu wa majimbo sita ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wachungaji na watumishi wa kituo hicho (hawapo pichani), kuhusiana na changamoto wanazozipata katika mashauri ya mirathi na ndoa katika kusuluhisha.