Watu 190 wamenusurika kwa ajali ya ndege Uturuki

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:57 AM May 10 2024
Ndege ya mizigo ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express.
Picha: Julia Nikhinson/REUTERS
Ndege ya mizigo ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express.

WATU 190 wamenusurika kifo nchini Uturuki baada ya ndege walikuwamo kupasuka tairi wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa wa Gazipasa. Wizara ya usafirishaji Uturuki imesema hakuna aliyejeruhiwa.

Kampuni yenye uratibu wa safari wa ndege hiyo aina ya Boing 737-800 ya shirika la ndege la Corendon la hukohuko Uturuki, imesema pamoja na tatizo hilo ndege ilifanikiwa kusimama uwanjani.

Ndege, ilikuwa na abiria 184 na wafanyakazi sita, ikitokea Cologne, Ujerumani. Shirika Corendon limekanusha ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitua kwa kutanguliza eneo la mbele, yaani pua yake. 

Katika tukio lingine la Jumatano ndege ya mizigo ya Boeing 767 mali ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express ilitua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul baada ya gia kushindwa kufanya kazi. Na kadhalika katika mkasa huo hakuna aliyejeruhiwa na wahudumu waliweza kufanya uokozi wa ndege hiyo salama.

DW