DRC, Rwanda vita yafukuta, EAC kuingilia kati leo

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 10:44 AM Jan 29 2025
DRC, Rwanda vita yafukuta, EAC kuingilia kati leo.
Picha:Mtandao
DRC, Rwanda vita yafukuta, EAC kuingilia kati leo.

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) leo Januari 29, inatarajiwa kuketi katika Kikao cha dharura cha wakuu wa mataifa katika juhudi nyingine za kuzuia vita kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda.

Hii inafuatia tuhuma za DRC kwamba Rwanda inafaidika kijasusi na kusaidia waasi wa M23 ambao wameanzisha mashambulizi katika mji wa Goma, Kongo.

Mashariki ya Kongo, ambayo ina rasilimali nyingi za madini, si mgeni kwa migogoro, ambapo vita vimekuwa vikikikabili taifa hilo kwa zaidi ya miongo mitatu.

Sehemu hiyo imekuwa uwanja wa vita kwa zaidi ya miaka 30. Kando na migogoro ya kikabila, inadhaniwa kuwa, ingawa si chanzo cha msingi cha mzozo, akiba kubwa ya madini katika Goma inawezkuwaa imeongeza makali ya vita vinavyozidi kudumu.

Goma, iliyo katika mpaka wa Rwanda na ufukwe wa Ziwa Kivu ambako ni kitovu muhimu cha biashara na usafirishaji cha karibu na wale wanaoshughulika na metali na madini, ikiwa ni pamoja na dhahabu, tin, na coltan.

Bado haijulikani iwapo Rais Felix Tshisekedi wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda watashiriki katika kikao hicho, kilichoitwa ili kujaribu kuleta amani katika Taifa hilo. 

Hata hivyo, Rais William Ruto amesema jana Jumann, Januari 28, kuwa wote Rais Tshisekedi na Kagame wamekubali kushiriki kikao cha leo.

Ingawa kikao cha leo hakiwezi kuleta mwisho wa papo hapo kwa migogoro ya miaka mitatu, kinatarajiwa kusaidia katika kuzuia hali isizidi kuwa mbaya na kupelekea vita kamili kati ya Rwanda na DRC.