WANANCHI wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, wametakiwa kutumia mvua za mwaka huu kama funzo ambalo litawafanya wajenge nyumba imara zitakazo weza kukabiliana na mvua ili kuepuka kujirudia kwa mafuriko ambayo yametoka mwaka huu na kusababisha nyumba nyingi kuanguka huku baadhi ya kaya zikikosa makazi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Kaya zilizokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Litapunga na Bulembo katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, huku Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Halawa Malendeja akisema mvua za mwaka huu ziwe kipimo cha kukabiliana na tatizo hilo.
Kwaupande wao wahanga wa mafuriko ambayo yemetokea siku za hivi karibuni katika vijiji hivyo wameiomba serikali kuendelea kuwashika mkono kutokana na mazingira magumu wanayoishi kwasasa kutokana na kuharibiwa makazi yao pamoja na mazao.
Misaada iliyotolewa katika kaya hizo ni vyakula, nguo, magodoro, mashuka na vinginevyo ambavyo vimegharimu zaidi ya shilingi millioni mbili.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED