Msafara wa Makonda wapata ajali

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 06:14 PM Feb 11 2024
Ajali kwenye msafara wa Katibu Mwenezi CCM, Paul Makonda.

MSAFARA wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Sululu Masasi mkoani Mtwara.


Ajali hiyo iliyotokea saa 9 alasiri imehusisha zaidi ya magari saba yaliyokuwepo katika msafara uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wasiopungua saba wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospital ya Mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote.