Luhaga Mpina atangaza kumpeleka mahakamani Waziri Bashe

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 01:55 PM Jun 30 2024
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina.
Picha: Maktaba
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina.

MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge ametangaza kupeleka malalamiko yake katika vyombo vya sheria kwa kuondolewa Bungeni kwa uonevu na kutokutendewa haki pamoja na Kumpeleka Mahakamani Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Bodi ya Sukari na kuyafikisha Mahakamani makampuni yote yaliyojihusisha na uingizaji wa sukari nchini kinyume na sheria.

Akiongea Jijini Dar es salaam, Mpina amesema “Baada ya kutafakari kwa kina mazingira na kilichotokea kwenye Kamati ya Bunge nimeamua yafuatayo moja kupeleka malalamiko yangu yakuondolewa Bungeni kwa uonevu na Spika wa Bunge kwenye vyombo vya sheria ili vikapime na kutoa haki kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za Nchi, pili kumpeleka Mahakamani Waziri wa Kilimo, hussein Mohamed Bashe na Bodi ya Sukari chini ya ibara ya 26 na ibara ya 27 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitendo cha kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha sheria na kulisababisha Taifa hili hasara kubwa tatu kuyafikisha Mahakamani makampuni yote yaliyo jihusisha na uingizajiwa sukari nchini kinyume na sheria”

“Nataka niwahakikishie Wananchi hakuna wa kunikatisha tamaa, nitaendeleza mapambano, sijawahi kushindwa, penye nia pana njia”