Kwa mara ya kwanza Duniani na kwa kushirikiana na @mastercard, Benki ya NMB (@nmbtanzania) imezindua rasmi mfumo wa malipo wa Lipa kwa QR link (QR pay by link with click to pay), ambapo wateja na wale ambao sio wateja wa NMB kutoka popote duniani wanaweza kufanya malipo kwa kadi zao kwa kuscan QR za NMB.
Mfumo huu utaongeza wigo wa malipo kwa wafanyabiashara nchini ambao hawajajumuishwa kwenye mifumo rasmi ya malipo
kama vile mashine za POS, ambapo wataweza kutumia “QR Pay by Link” kama mbadala wa mashine za POS.
Sasa ukifika dukani, sehemu za bata, kwenye usafiri na sehemu yoyote ya malipo, scan QR link na utafanya malipo kupitia simu yako, na kuhifadhi taarifa zako kwa usalama ili uendelee kufanya malipo.
Uzinduzi huu umefanywa mbele ya Mwakilishi Mkazi wa Mastercard Kanda ya Afrika Mashariki, Shehryar Bahk Ali aliemkabidhi tuzo maalumu Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi inayoitambua NMB kama Benki ya kwanza Afrika kuja na suluhusho hili. Mgeni rasmi katika tukio hili alikua Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Aboud Suleiman Jumbe.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED