Idadi ya waliojiandikisha wafiia milioni 26, Mchengerwa asema siku hazitaongezeka

By Julieth Mkireri , Nipashe Jumapili
Published at 09:25 PM Oct 20 2024
Idadi ya waliojiandikisha wafiia milioni 26, Mchengerwa asema siku hazitaongezeka
Picha: Mpigapicha Wetu
Idadi ya waliojiandikisha wafiia milioni 26, Mchengerwa asema siku hazitaongezeka

WATANZANIA Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81.15 ya walengwa wamejitokeza kujiandikisha daftari la makazi hadi kufikia Oktoba 19 jioni.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa alipokuwa akizungumza na  baada ya kujiandikisha katika kituo cha kupigia kura  Ikwiriri wilayani Rufiji.

Mchengerwa amesema idadi hiyo ni tangu uandikishaji uanze Oktoba 11 hadi 19 jioni ambapo leo ndio tamati itafikiwa na taarifa ya jumla itatolewa usiku wa saa sita.

Waziri huyo amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 81.15 ya lengo la uandikishaji wapigakura 32987579 kwa siku zote kumi zilizotengwa kutumika kuandikisha wapiga kura.

" Kati ya watu hao waliojiandikiah Wanawake ni Milion 13,033,988 ni wanaume sawa na asilimia 48.69 huku Wanawake wakiwa  Miln 13,736,007 sawa na asilimia 51.31 uwezekano wa kufikia malengo ya uandikishaji utakuwa mkubwa hadi mwisho wa siku ya leo," amesema Mchengerwa.

Aidha amebainisha kwamba kumekuwa na ongezeko la wananchi kujiandikisha kuanzia siku ya tano hadi ya tisa tangu Uandikishaji uanze .

Ameitaka mikoa mitano inayoongozwa kwa kuandikisha watu wengi kuwa ni Tanga ambayo imefikia asilimia 101.13, Pwani 98.74, Mwanza 94.09, Dar es Salam 86.66 na Dodoma 80.63.

Mchengerwa amesema siku zilizopangwa zikiisha hakutakuwa na kuongeza muda wa kuendelea kuandikisha .