KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, anatarajia kutoa kauli kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa mustakabali wa nchi.
Dorothy atatoa kauli katika mkutano na waandishi wa habari, makao makuu ya chama, Magomeni Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama.
Naibu Mwenezi wa chama Shangwe Ayo, amesema Kamati ya ACT Wazalendo ilikutana jana, kwa ajili ya maandalizi ya Halmashauri Kuu hiyo inayokutana leo saa nne asubuhi.
Kamati Kuu ya Chama cha ACT- Wazalendo ilikutana jana katika kikao cha Maandalizi ya Halmashauri Kuu ya Chama na sasa.
"Kiongozi wa chama, Dorothy Semu atatoa hotuba kwa waandishi wa habari kwenye ufunguzi kikao cha Halmashauri Kuu," amesema Shangwe.
Bila kufafanua, Shangwe amesema kuna mambo mazito yahusuyo nchi ambayo Kiongozi huyo wa chama atayatolea kauli kwenye Halmashauri Kuu.
"Hivyo, waandishi mnakaribishwa kuja kumsikiliza kiongozi wetu wa chama akielezea yale ambayo kamati kuu imefikia katika chake cha jana," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED