INAPOANGALIWA Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050 iliyotolewa mnamo mwezi Desemba mwaka jana, inaangazia ifikapo safari yake, kuna malengo:
Inagusia Tanzania inayotarajiwa kuwa taifa lenye maendeleo yanayolingana na nchi zenye uchumi wa Kipato cha Kati, Ngazi za Juu na zaidi.
Rasimu hiyo inaweka wazi kuwa, ili kufikia hatua hiyo, kunahitajika mageuzi makubwa ikizingatiwa kuwapo ongezeko kubwa la watu wanaokadiriwa kufika milioni 140.
Kati yao, nusu ya idadi hiyo watakuwa wanaishi mijini na inatarajiwa wengi wao watakuwa ni vijana.
Mbali na makadirio hayo, hata leo ikirejewa Sensa ya Watu a Makazi ya Mwaka 2022, takwimu inaonesha idadi ya vijana kuwa kubwa, asilimia 34.5 ya Watanzania wote.
Moja ya eneo ambalo ni Mpango wa kuhakikisha kunafikiwa ‘Tanzania Tuitakayo’ kama ilivyotolewa Desemba 2024 kwenye dira hiyo ya maendeleo kusonga 2050,
ni pamoja na kuwapo "ubora wa hali ya juu wa maisha na ustawi kwa wote.”
Msingi wake ni kwamba, hakuna namna nyingine ya kuwa na ubora, bila ya kuwapo uvumbuzi na ubunifu. Kufikia ustawi huo, ni lazima ubunifu uweze kupewa nafasi kubwa ya kukuzwa katika kundi kubwa la watu linalotarajiwa kuongezeka kwa kasi wakati huo, likijumuisha vijana.
Ikirejewa nukuu za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akatamka "ujana ni siha njema na bongo kali." Hapo alimaanisha kwamba, vijana hao wana uwezo mkubwa wa kufikiria.
Hivyo wana wajibu wa kutumikia fursa mbalimbali na kuonesha ubunifu walionao, pindi wanapopewa ushirikiano mkubwa na serikali, ili kuhakikisha “tunafikia Tanzania tuitakayo hata kabla ya 2050.”
Ni jambo linawezekana kupitia uvumbuzi na ubunifu, ikiwa sehemu ya vichocheo muhimu vya maendeleo yao vijana, pia uchumi kwa maendeleo endelevu.
Kwa kuzingatia uwapo wa idadi kubwa ya vijana, suala la uvumbuzi na ubunifu linapaswa kupewa kipaumbele katika sera na mipango, kwa maslahi mapana ya vijana na maendeleo ya taifa.
Ni msingi unaozipa serikali na wadau, wajibu wao wa ulezi na usimamizi, kuhakikisha kwamba vijana wanawezeshwa kwa kupatiwa ujuzi stahiki wa kuvumbua.
Pia, watakuwa wanabuni na kuibua kuibua vipaji hiyo, vishiriki kikamilifu katika elimu na uchumi unaoendeshwa na uvumbuzi na ubunifu ambao ndiyo msingi wa Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.
ENEO LA PILI
Eneo la pili linalohitaji ubunifu mkubwa, hasa kutoka vijana walipo katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050, ikihitaji usimamizi thabiti na endelevu wa ikolojia.
Vijana hapo wanapaswa kuwa wabunifu katika kuhakikisha ongezeko la uchafuzi wa mazingira na upotevu wa baadhi ya aina za viumbe hai kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, yanapewa ufumbuzi na kutatuliwa.
Kundi hilo la vijana linanapaswa kuitikia kwa nguvu, ikibuni, kuvumbua na kuboresha njia za kuhakikisha ikolojia inabaki sawia, kuvipa viumbe vyote nafasi ya kuzaliana na kuongezeka.
Hapo inaendana na kupitisha vinasaba kwenye vizazi vijavyo, vikitunza ikolojia katika ngazi yake sawa, ndipo hata maisha ya binadamu na uzalishaji utazidi katika viwango vikubwa.
Kwani ndani ya ikolojiam ndiko kunapatiokana malighafi za kulisha viwanda vikubwa na vidogo, huku uchumi ukizidi kukua.
Jukumu la kufikia malengo yote ya Tanzania ‘tuitakayo mpaka kufikia mwaka 2050’ ni la watu wote, hata mwitikio wa vijana katika ubunifu ukiwa mkubwa bado watahitaji kupewa ushirikiano na serikali pamoja na jamii kwa ujumla.
Inajulikana, serikali ipo tayari kutoa ushirikianao mkubwa kwa vijana wanapokuwa na ubunifu wenye kuleta maendeleo ya taifa. Mfano hao unapatokana hata kuoptia majukumu ya taasisi ya kitaifa ya COSTECH, ambayo majukumu yake ya kila siku yamesimamia ngazi hiyo.
Pia umma, wakiwamo vijana, wana wajibu muhimu kuhakikisha wanadumisha amani na kuwapa nafasi ya kufanya ubunifu mbalimbali kama wana jamii, ilimradi wanayolibuni itufikishe kwenye “Tanzania Tuitakayo.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED