Zitto: Bandari ya Mbamba bay ni ya kimkakati iharakishwe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:10 PM Sep 13 2024
Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametuma salamu kwa Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa kumtaka afuatilie na kuhakikisha Mradi wa Bandari ya Mbamba bay unakamilika ili kuchochea uchumi wa Ruvuma.

"Tumechoka kusikia kila siku mkandarasi yupo site tunataka bandari ikamilike. Tukikamilisha Ujenzi wa Bandari ya Mbamba bay na ijengwe Reli kutoka Bandari ya Mtwara mpaka Mbamba bay uchumi utakua maradufu."

"Kujenga Reli kutoka Mtwara mpaka Mbamba bay, kubeba makaa kwenda Mtwara, barabara hazitabomoka, Afya za wananchi zitakuwa nzuri, mzigo wote wa Malawi utapitia Bandari ya Mtwara na Mbamba bay na mwengine kwenda Zambia na sehemu ya Msumbiji. Tunataka Bandari ya Mbamba bay iwe ya kimkakati"

Zitto ameyasema hayo jana Septemba 12, 2024 alipokua akihutubia mamia ya watu Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.