Uwekezaji wa serikali ulete matokeo chanya Sekta ya Afya

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:41 PM Sep 17 2024
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,  Dk. Denedicto Ngaiza.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Denedicto Ngaiza.

Madaktari bingwa na Bingwa Bobezi wapatao 64 wa Mama Samia walioanza kambi mkoani Mtwara wametakiwa kuwa chachu ya huduma bora za afya kwa siku zote tano watakazoweka kambi mkoani humo.

Madaktari bingwa na Bingwa Bobezi wapatao  64 wa Mama  Samia walioanza kambi mkoani humo wametakiwa kuwa chachu ya huduma bora za afya kwa siku zote tano watakazoweka kambi mkoani humo.

Hayo yamebainishwa na jana Septemba 16, 2024 mkoani Mtwara na  Mganga Mkuu wa mkoa huo,  Dk. Denedicto Ngaiza  akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bahati  Geuzye, wakati wa ufunguzi wa Kambi ya awamu ya pili ya Madaktari bingwa na Bobezi iliyopo mkoani humo kuanzia leo.

Madakatari hao waliowasili mkoani humo wanatarajiwa kutoa huduma kwenye Halmashauri zoate tisa.
   
“Mbali ya jukumu kubwa mlilonalo lakutoa huduma kwa wanaanchi, tumieni fursa hii pia kuwajengea uwezo wataalamu wenzenu katika ngazi ya msingi ili kuhakikisha wananchi wa ngazi ya msingi wanapata Huduma bora, stahiki na kwa wakati”, amesisitiza Dk. Ngaiza.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi Afisa Programme kutoka Wizara ya Afya, Celphlen Budodi, amesema huduma zitakazotolewa na Madaktari bingwa  ni pamoja na  magonjwa ya watoto, wanawake na uzazi, kinywa na meno, dawa za usingizi na ganzi, uuguzi na ukunga, magonjwa ya ndani, upasuaji na njia ya mkojo, pamoja na mifupa  na kwa hospitali ya Manispaa ya Mikindani Mtwara.

" Wakati wa zoezi hilo wananchi wameombwa kuchangia gharama kiasi  huku akisisitiza wenye bima za afya kuwa nazo  kwaajili ya kupata matibabu hayo kutoka kwa madaktari bingwa na bingwa bobezi" amesema Budodi

Kwa upande wao Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka hospitali ya Perahimo mkoani Ruvuma, Dk. Monica  Mboka  amesema kuwa  huduma hiyo wanaitoa kwa mara ya  pili ikiwa ni muendelezo uliosukumqa na mwamko wa awamu ya kwanza.

Naye Daktari Bingwa wa upasuaji toka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk. Dino Simoni amewahaidi wananchi kutoa huduma bora huku akiweka bayana kuwa watakuwa na madaktari bingwa wa mgonjwa ya meno ambapo hapo awali hawakuwepo.

Madaktari Bingwa wa Mama Samia watakuwepo kwenye mkoa huo kwa muda wa juma zima ikiwa ni muendelezo wa kambi iliyofanyika mapema mwezi Mei hadi Juni, 2024.