Kamishna TRA ampatia zawadi mfanyakazi aliyepongezwa na wafanyabiashara

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 06:56 PM Sep 17 2024
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) CPA.Yusuph Mwenda
Picha:Shaban Njia
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) CPA.Yusuph Mwenda

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) CPA.Yusuph Mwenda amelazimika kumpatia zawadi mfanyakazi wake kutoka Ofisa ya mkoa wa kikodi Kahama Ismail Mwaipaya baada ya kusifiwa na wafanyabiashara kutokana na huduma anazowapati wanapofika ofisini kupata huduma pasi kuwaomba rushwa.

Mwenda amempatia zawadi ya Sh.milioni moja, cheti cha pongezi ambacho kitawekwa kwenye faili lake na zawadi yatatu ataangalia namna ya kumpandisha cheo na kuwataka wafanyakazi wengine kuingia mfano wake ili nao waje wasemewe vizuri na wafanyabiashara kikao kijacho.
 
Zawadi hizo zilitangwa mbele ya wafanyabiashara wadogo, wakati, wakubwa pamoja na watumishi wa Mamalaka ya Mapato mkoa wa kikundi kahama wakati wa kikao kazi cha kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na kuzitafutia ufumbuzi wake ili kulipa kodi pasi kuvutana.
 
Amesema,watumishi wake atakuwa anawapima kwa utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya walipa kodi, kwani mpaka sasa kahama inajumla ya walipa kodi 24,000 na hao ndio wanaofika ofisi hiyo kufanya vema katika kukusanya kodi kulinganisha na mikoa mingine.
 

1

Mwenda amesema,kila mwaka Ofisi yake imekuwa ikitoa zawadi kwa Mameneja ambao wamekuwa wakifanyavema kwenye kukusanya kodi na sasa anaongeza zawadi ya viongozi ambao wamekuwa wakihamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kama ambavyo anafanya Mkuu wa wilaya ya kahama Mboni Mhita.
 
Miongoni mwa wafanyabishara Hamisi Mgeja amesema, mfanyakazi Isimail Mwaipaya anafaa kupewa zawadi kutokana na huduma ambazo amekuwa akizitoa kwa wafanyabiashara bila kutumia nguvu ya aina yoyote na pale inapohitaji ufafanu anakuelewa na kuelewa.

2

Hoja ya kupewa zawadi iliunga mkono na wafanyakazi wenzie na kudai amekuwa akijituma sana katika kazi huku wengine wakihusisha na imani yake ya kuwa muislamu kwani ibada ameiweka mbele na kuwa na hofu na Mungu na ndio sababu ya kuwa na kauli nzuri kwa wateja na kutojihusisha kwenye vitendo vya rushwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita nae aliridhia kwa mfanyakazi huyo kupewa zawadi kwani hajawahi kupata malalamiko yake ya aina yoyote kulinganisha na wengine, na wale wanaolalamikiwa amekuwa akitoa taarifa zao na kuwachukuliwa hatua za kiutumishi.

3