Wanaopokea matangazo kupitia visimbuzi wafikia milioni 12 nchini

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 12:27 PM Jun 17 2024
news
Picha: Maktaba
MENEJA wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka.

MENEJA wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka (pichani), amesema inakadiriwa watu wanaotazama televisheni kupitia visimbuzi wanafikia milioni 12.

Amesema nchini kuna visimbuzi milioni 3.8 huku ikikadiriwa kila kaya ina wastani wa familia nne, hesabu ambayo ikizidishwa na idadi ya visimbuzi watumiaji wanakadiriwa kufikia milioni 12 nchini.

Kisaka, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, mkoani Dar es Salaam, akiwasilisha mada kuhusu Wajibu na Majukumu ya Vyombo vya Habari Kuelimisha Umma na mchango wa vyombo vya habari kama vile televisheni katika kuelimisha umma;

Katika mkutano ulioandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji daftari la kudumu la wapigakura awamu ya kwanza, ukiwakutanisha waandishi wa habari takribani 200 wa mkoa huo.